Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa @nic_insurance , Bw. Karimu Meshack, akielezea namna NIC Insurance Ilivyofanya mapinduzi makubwa katika sekta ya bima nchini wakati wa Kongamano la Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano na Masoko wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha.
NIC Insurance imefanikiwa kuongeza faida ghafi kutoka shilingi bilioni 33.65 mwaka 2019/20 hadi shilingi bilioni 63.21 mwaka 2021/22 sawa na asilimia 43.91 kwa mwaka. Aidha, kutokana na faida mfululizo NIC imeweza kupata malimbikizo ya faida ya Shilingi bilioni 45.74 kufikia Juni, 2022 kutoka kiasi cha malimbikizo ya hasara ya shilingi bilioni 19.31.
Kwa mwaka ulioishia Juni, 2022 NIC imetoa gawio la shilingi bilioni 2.0 Serikali ikilinganishwa na gawio la kiasi cha Shilingi bilioni 1.5 lililotolewa mwaka ulioishia Juni 2021, huku wakifanikiwa kuongeza mtaji wa kiasi cha shilingi bilioni 12.05 mwezi Aprili, 2022 sawa na ongezeko la asilimia 408.47 kutoka mtaji uliokuwepo wa kiasi cha shilingi bilioni 2.95 na kufikia mtaji wa kiasi cha shilingi bilioni 15 kilichopo sasa.
#NICat60 #Sisindiyobima #superbrands #nicinsurance #isocertified90012015