NIC Insurance imeibuka mshindi wa pili wa tuzo ya umahiri katika uhusiano mawasiliano kwa mwaka 2023 kwenye kipengele cha kudhibiti na kupambana na majanga (Issues and Crisis Management". Tuzo hizi za Umahili (Public Relations and Communication Excellence Awards) za PRST zilitolewa tarehe 5/04/2024 kwenye Ukumbi wa St. Peters jijini Dar es Salaam na Mgeni Rasmi alikua Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Technolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi. NIC inawashukuru watu wote waliofanikisha kwa namna moja ama nyingine ushindi wa tuzo hizi.