Success, we'll get back to you
Back to news

NIC Insurance na benki ya Equity imezindua rasmi ushirikiano wa bima nafuu kwa wakulima na wafanyabiashara

SHARE

NIC Insurance na benki ya Equity imezindua rasmi ushirikiano wa bima nafuu kwa wakulima na wafanyabiashara. Kupitia ushirikiano huu, mashirika haya yanalenga kutoa suluhisho za kifedha za kidijitali, kulinda mali na mitaji ya wateja wetu dhidi ya majanga kama moto, wizi, na ukame


“Hii ni moja ya njia ya uwekezaji tunawekeza kazika benki za kibiashara ambazo zipo hapa nchini ili ziweze kuwa na uwezo wa kukopesha na kila mmoja wetu anajua ukwasi ni muhimu sana katika benki hizi za biashara ili wananchi wetu, kampuni zetu za hapa, wawekezaji mbalimbali wanaokuja nchini waweze kukopesheka na mwisho wa siku tuweze kufanya shughuli za kiuchumi bila kutetereka.


“Ukiliangalia jambo hili ni kubwa kwa hiyo sisi tutaingia makubaliano yatakayoiwezesha Equity Benki kuwa na mtaji mzuri na kuongeza mtaji wao na tunajuwa wano na vilevile umuhimu wetu kwetu ni kuwekeza kwao lakini pia vilevile na sisi kupata marejesho yanayotokana na uwekezaji wa fedha hizo lakini pia kuna faida za ziada sisi tutapata kama yeye ataweza kukopesha kwa uwezo tuliompa sisi basi na sisi tutatumika kama kampuni itakayokata bima za mikopo ambaye atakuwa anakopesha kwa hiyo apo utaona ata mikopo anayokopesha itakatiwa bima” Amesema Abdi Mkeyenge (Mkurugenzi Mtendaji - NIC INSURANCE)


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Isabela Maganga amesema benki inapofanya kazi ya kutoa huduma za bima haiwezi kufany kazi peke yake ni lazima washirikiane na taasisi za bima ambazo zenyewe zina wigo mpana na wigo mkubwa katika kutoa huduma hizo .


“Sasa kwa kutambua ukubwa huo na uwezo huo wa shirika la Bima la Taifa (NIC) sisi Equity Benki tukasema tuwe na mahusiano ya kimkakati ambayo taasisi zetu mbili tunaweza tukafanya kazi pamoja na katika kuanzisha mahusiano hayo ya kimkakati tumeangalia huduma ambazo sisi tunazitoa ndani na tumezipa kipaumbele zina uhitaji mkubwa wa wateja na zina uhizaji mkubwa wa soko.

“Katika kuangalia hilo tumeona kwa sasa hivi kama benki tumeipa kipaumbele sekta ya kilimo lakini katika madaraja ya wateja tumetoa kipaumbele sana kwa wafanyabiashara wadogo na wakati ambao wateja hawa katika kutoa huduma kwa sisi tunawafikia kwa njia ya kidigitali katika kuwawezesha kupata mitaji ” amesema Isabela

Share

Tweet

Share