Success, we'll get back to you
Back to news

WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI YA NIC INSURANCE WATEMBELEA MKOA WA KAGERA

SHARE

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NIC Insurance wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Bw. Justine Mwandu amefanya ziara Mkoa wa Kagera kwa lengo la kukagua mali za Shirika na kujionea namna NIC inavyoendelea kutoa huduma mbalimbali za bima kwa wananchi


Ziara hii ilianzia kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatuma Mwasa ambapo aliweza kuzungumza na wajumbe wa bodi na kuwakaribisha rasmi Mkoa wa Kagera


Mkuu wa Mkoa wa Kagera amesema “Jamii bado haijatambua umuhimu wa kuwa na bima mbali na kuwa na gharama za chini za ada za bima kama bima za nyumba”


Mwenyekiti wa Bodi ya NIC Insurance Bw. Justine Mwandu amemhakikishia mkuu wa mkoa wa Kagera kuwa NIC Insurance itaendelea kushirikiana na serikali ya mkoa kutoa elimu na huduma za bima kwa makundi mbalimbali mkoani Kagera