Mkurugenzi Masoko na Mawasiliano wa NIC Insurance Bw. Karimu Meshack amekabidhi fanicha na vifaa tiba vyenye thamani ya sh. Million 20 kwa Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Dkt John Rwegasha kusaidia maboresho ya huduma za afya kwa watoto katika hospitali hiyo.
Kwa upande wake Dkt Rwegasha ameishukuru NIC Insurance kwa msaada huo kwani usaidia kuboresha huduma za afya na kuimarisha utoaji wa huduma kwa Watoto na Sekta ya Afya kwa ujumla.