Success, we'll get back to you
Back to news

NIC Insurance yadhamini Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kwa Klabu ya Yanga

SHARE

Ushirikiano wetu na Klabu ya Yanga ambazo tumekuwa wadhamini rasmi wa ‘Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi.’ Udhamini huu ni utadumu kwa miaka mitatu, kuanzia msimu huu wa 2023 mpaka 2026.

 

Ushirikiano huu unazikutanisha taasisi mbili zenye historia kubwa ya ufanisi na weledi Tanzania ambapo NIC Insurance ni kampuni ya serikali ikiwa na uzoefu wa miaka 60 ya utoaji wa huduma mbalimbali za bima kwa Watanzania wakati Yanga ni klabu kongwe na mabingwa wa kihistoria katika mpira wa miguu nchini.

 

Dhumuni kuu la NICInsurance kuamua kuingia ushirikiano huu ni kuunga mkono vilabu vya ndani kama Yanga pamoja na sekta nzima ya michezo. Tunaamini kuwa ushirikiano huu utaleta chachu kwa wachezaji wa Yanga kujituma zaidi na kuonyesha ubora wao kwa timu na kila mechi kuisaidia timu yao huku mwisho wa mwezi wakiwa na uhakikwa wa kupata

zawadi kutoka kwetu.

 

“Huwezi kuzungumzia BIMA bila kuitaja NIC, na katika soka Yanga ni nembo ya soka kwa Tanzania akiwabingwa wa kihistoria. Tunayo furaha kubwa kupata fursa ya kufanya biashara na taasisi kubwa kama hii. Kwa upande wetu NIC imepewa hadhi ya kuaminika”

- Dkt. Elihuruma Doriye – Mkurugenzi Mtendaji NIC Insurance