Success, we'll get back to you
Back to news

NIC KUENDELEA KUBORESHA NA KUBUNI HUDUMA MPYA ZA BIMA

SHARE

NIC Insurance katika kutimiza miaka 60 imesema itahakikisha inaendelea kuboresha huduma zake kwa kubuni huduma mpya lakini kushirikiana zaidi na jamii ili kuhakikisha elimu ya Bima inamfikia kila mmoja.

Hayo ameyasema leo Oktoba 16, 2023 Mtendaji Mkuu wa NIC Elirehema Doriye wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao kilichowakutanisha na watendaji wakuu wa timu ya yanga na wachezaji.

Amesema maadhimisho ya miaka 60 ya shirika hilo yamekua ya manufaa makubwa kutokana na juhudi zinazofanywa na serikali katika kuliinua na kuliendeleza shirika ili kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na Bima.


“Leo tunaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa shirika hili ambapo tunajivunia mafanikio makubwa ambayo tumeyapa kwa kipindi chote lakini pia tumekuja na mikakati itakayosaidia katika kuandaa miaka mingine 60 ijayo”amesema Doliye.

Amesema moja ya vipaumbele ambavyo wameviweka ni kuhakikisha wanawekeza kwenye TEHAMA kwa kuwa wabunifu zaidi kwa kubuni huduma ambazo zitabaki kwenye mioyo ya wateja kwani itakuwa kampuni ya kwanza kutumia akili bandia katika utendaji wake.

Amesema wataendelea kukuza biashara ndogo ndogo kwa kwa kupanua wigo wa kutoa huduma kwa wananchi.

Aidha Doriye ameongeza kuwa kuunga mkono vipaumbele vya serikali ikiwemo katika sekta ya kilimo kwa kutoa Bima ya kilimo.

Sambamba na hayo Doriye amesema kuwa wataendelea kuwa karibu na jamii kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo katika sekta ya Afya na mazingira.

“Hii ni Bima ya wanachi na tupo kwenye maazimisho ya miaka 60 lakini pia kuandaa miaka 60 ijayo tumejidhatiti kutoa elimu kwa wananchi lakini kushirikiana na wananchi hivyo tutakua na mabonanza mbalimbali ya michezo yatakayohusisha sekta binafsi na serikali wakiwemo waandishi wa habari”ameongeza Doriye.

Amesema wanatarajia pia kufanya mazungumzo ya kitaaluma ili kuhakikisha elimu ya Bima inamfikia kila mtu lakini pia kuandaa video yenye historia ya Bima.

Aidha Doriye ameongeza kuwa yote watakayoyafanya kama maazimisho ya miaka 60 watashirikiana na timu ya mpira wa miguu ya Yanga.

Nae,Mtendaji Mkuu wa klabu ya Yanga Andre Mtine ameishukuru NIC na kuahidi kushirikiana nao katika kuhakikisha elimu ya Bima inamfikia kila mtu lakini pia kushirikia katika shughuli za kijamii ikiwa kama sehemu ya kutoa elimu.

“Sisi kama Yanga tunafurahia kuwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya NIC kwani hii ni taasisi ya kwanza ya Bima na inafanya vizuri sana sisi tunaahidi kushirikiana nao”amesema mtine.